WATANZANIA NA MAFANIKIO YA HARAKA!

December 14, 2007 by Maka Patrick

Waliosema kuwa usione vyaelea vimeundwa waliona mbali sana!Leo sitaki kuandika mengi bali nawaeleza Watanzania wapenda soka wanaoitakia mema timu yao ya Taifa,pia timu yao ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kuwa mafanikio hayaji siku moja,mafanikio hayaji kwa kuwataka wachezaji ambao kocha hajawachagua bali washabiki,wapenzi wanawang’ang’ania na kuwaona kuwa ndiyo watakaoleta mafanikio!Watanzania wapenda soka nawaomba sana jamani kuwa tusipende mteremko!Mnadai kuwa timu ya Kilimanjaro haifanyi vizuri mara mnawazomea wachezaji pmoja na kocha lakini mmesahau kuwa timu hiyo ni changa na je ni wapi mliona kuwa timu changa inafanikiwa kwa haraka kiasi hicho?Mechi ngapi za majaribio tumcheza?Si moja tu halafu nasema kuwa oohoo hii timu inatupa shinikizo jamani shinikizo lipi mlipatalo kwa timu chnga kama ile?Haya ni mambo ya kusubiri timu ndiyo inajengwa!Wala msiwe na ndoto kuwa tutachukua chalenji timu yetu bado tuchukulie mechi hizi kama za majaribio wakati wenzetu wanaona ni mashindano sisi iwe kwa ajili ya kuijenga timu yetu kwa michuano ya baadaye tusitazame hapa tutizame mbele zaidi matunda tutajayapata baadaye si kwa muda huu mfupi kumbukeni kuwa tupo kwenye kipindi cha mpito!Asanteni.

WATANZANIA KUNDI LETU NDILO GUMU WALA SI RAHISI!

November 29, 2007 by Maka Patrick

Kuna baadhi ya watu wameanza kuwadanganya watanzania nasi watanzania ni wepesi wa kuamini mambo ambayo kwa hakika huwa si ya kweli kabisa!Kumbuka jinsi watu walivyokuwa na matumaini ya kwenda Ghana kila mmoja alijua kuwa mwakani sote macho yetu kideoni tukiwashangilia Stars na Stars nao masikini wakaanza kuvimba vichwa wakati hata safari bado ilikuwa mbichi kabisa!Kumbuka jinsi walivyokuwa na nyodo wakati wanakwenda kucheza na Zambia kule mji unaotamani angalau kuwa na bahari japo kwa siku moja,Morogoro,washabiki waluguru wale wamefika Msamvu kuwalaki wachezaji wao lakini Stars wakawafungia vioo maana tayari wao wameishakuwa wafalme!
Ninachotaka kusema siyo kukatisha tamaa la hasha bali kuwaasa watanzania wenzangu kuwa kundi letu si rahi ni gumu sana na pengine ndilo kundi gumu kuliko makundi yote katika safari hii ya kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia.
Tukumbuke kuwa kwa soka la kisasa hakuna kitu kinachoitwa timu rahisi au kundi rahisi kama nilivyosema jana kuwa mpira ni mchezo wa maandalizi kama mitihani,mpira ni mchezo wa kujitoa,kujituma,kupambana na si kucheza soka ya midomoniambayo ndiyo tunayoiweza watanzania.Mpira ni burudani lakini kwa upande mwingine mpira ni vita tena ni vita kubwa sana sana.Sitaki kuongea mengi leo maana nitakuwa kama nimemeza kanda na maneno yanajirudia yaleyale.Kwa kifupi tuache maneno tuanze maandalizi sasa wakati ni huu na wala hatujachelewa.Asanteni sana na ni matumaini yangu kuwa sote kwa pamoja tutashikamana na kuanza maandalizi sasa.

CAMEROUN WANAFUNGIKA IWAPO TU……………

November 28, 2007 by Maka Patrick

Wasomaji wangu wapendwa kwanza naomba niwaombe radhi kwa kutokuwepo hewani kwa takribani mwezi hivi hii yote inatokana na kuzidiwa na majukumu.Naomba radhi sana kwa hilo.Najua dada Salome wa Mtibwa Sukari,Deogratius Zegge wa Serena pale Tengeru Arusha na Mwandishi wa siku nyingi wa “gazeti la Daily Vision” la Kantalamba Sekondari pale Sumbawanga 1991-1993 bwana Boaz A. Boaz mtakuwa menisamehe baada ya kuwa sijaonekena kwa muda mrefu kidogo.
Leo nataka nizungumze juu ya kupangwa kwa ratiba ya kombe la dunia Afrika Kusini 2010 kule Afrika ya Kusini.Tupo kundi la kwanza katika kanda hii ya Afrika pamoja na vinara Cameroun,Visiwa vya Cape Verde na Mauritius.Kimahesabu kundi letu ni kama rahisi sana lakini kimchezo ni kundi la kati au wastani au kundi la kama watu wengine waonavyo la hizi timu tatu kuwa wasindikizaji wanaomsindikiza mfalme Indomintable Lions.
Mpira ni mchezo wa maandalizi,juhudi,maarifa kujitoa,kujituma na pia mchezo wa makosa.Cameroun wanajielewa kuwa wao ni wababe lakini kamwe hawawezi kjidanganya kuona kuwa timu kwazo walizopangiwa nazo ni vibonde.Tukumbuke kuwa hawakuwepo Ujerumani na wanalitambua hilo na wanajua machungu ya kukosa kushiriki fainali hizo kwa wao kukosa penati nyumbani.Hawatakubali kufungika na wanaweza kuwa na hasira sana hasa ukizingatia kuwa hwakuwepo katika fainali zilizopita kama kawaida yao.Hawawezi kukubali wazikose fainali hizi tena zinazochezwa katika bara hili la hapa nyumbani.Kwa kifupi Wana Wa Cameroun wanatambua kuwa kundi walilopangwa nalo kwa soka la siku hizi si timu vibonde hivyowako tayari kupigania nafasi yao kuliko vile watu wengine wafikiriavyo kuwa wamepangiwa timu vibonde!Wana EWa Cameroun wataingia kupigana na wanajua kuwa nguvu ya adui zao ni kubwa kutokana na soka la siku hizi kuwa limekuwa sana.Halikadharika hizi timu zingine pia zinajua kuwa yupo mfalme wa kundi nasi pia tujitahidi tuzifunge timu zingine!Kifupi kundi letu kila timu inapiga hesabu za kivyakevyake ili waweze kufanikiwa.
Ninachotaka kusema ni kuwa Cameroun wanafungika lakini wanafungika tu iwapo tutaanza maandalizi mapema tutaanza maandalizi sasa hivi tutaanzana maandalizi leo na wala siyo kesho!Cameroun atafungika tu iwapo tutaacha malumbano ya kuwa wachezaji gani ni bora na wachezaji gani siyo bora!Cameroun atafungika tu iwapo tutashikamana wote na pia tutampa mwalimu sapoti kubwa sisi sote kama watanzania na tunoitakia mema timu yetu.Maandalizi yaanze sasa kupata mafunzo nje ya nchi,kupata mechi za majaribio kutokukata tamaa sote lazima tushikamane kwa umoja wetu tutaiweza safari ya Afrika Kusini na Angola 2010 na hakika tunaweza kuishangaza dunia.Watanzania hakuna lisilowezekana katika sayari hii ni mipango madhubuti na mikakati ya maana tu ndiyo itakayoweza kutukomboa kutoka katika utumwa wa kuwa wasindikizaji.”TUJIKWAMUE SISI WENYEWE KUTOKA KATIKA MAWAZO YA KUWA WASINDIKIZAJI HAKUNA ATAKAYETUFANYA KUWA HURU ILA NI SISI WENYEWE!”
Boaz,Salome na Deo nisaidieni kuwaeleza watanzania kuwa haya mambo yanawezekana iwapo tutakuwa na maandalizi ya maan akutoka sasa.Naomba mnisaidie kuwaeleza watanzania wote!Nisaidieni kwa njia mbalimbali kwa kupiga kelele kwa vipeperushi,kwa kuwajulisha watu mbalimbali na kwa kutumia njia zozote zile kwazo zinafaa kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania.Kombe la dunia inawezekana!TWENDE TUJIANDIKISHE SASA WAKATI NI HUU!
Mwaka 2010:
Nchi:Afrika Kusini
Mji:J’burg
Uwanja:FNB Stadium
Kundi A:Mabingwa Italy,Spain,Japan,Tanzania
Mechi ya ufunguzi:Mabingwa Italy vs Tanzania
Matokeo ya mechi:Tanzania 1-Italy 1.
Tanzania leo imetoka sare na mabingwa wa dunia Italia kwa kufungana bao 1-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa First National Bank mjini J’burg katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa kombe la dunia hapa katika bara la Afrika.Ikumbukwe kuwa nchi hii ya Tanzania ndiyo mara yake ya kwanza kushiriki fainali hizi za kombe la dunia na pia ndiyo mabingwa wa kombe la Afrika kwa mwaka huu walilolitwaa mapema mwaka huu katika fainali za mataifa huru ya Afrika huko Angola baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Misri huko mjini Luanda Angola.Mechi zijazo za Tanzania ni dhidi ya Japan na halafu itamalizia mechi zake kwa kupambana na Spain.
Hya mambo jamani yanawezekana ni suala la maandalizi tu na mipango madhubuti.Hakika inawezekana kama tumedhamiria na kama kweli tunataka kuwa washindani wa kweli.Asanteni sana na shime tuanze maandalizi sasa wakati ni huu bado hatujachelewa.

JAMANI CHONDECHONDE ETI SIMBA NA YANGA NGOMA ITAPIGWA USIKU UWANJA MPYA!

October 12, 2007 by Maka Patrick

Nimeshtushwa sana na habari kuwa mechi ya watani wa jadi itapigwa uwanja mpya wa taifa siku ya tarehe 24 mwezi huu usiku.Kwa kweli nimeingiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hiyo mechi kupigwa katika uwanja ule mpya na wa kisasa zaidi,kwa nini ninakuwa na wasiwasi na hiyo mechi ni kuwa ninaaelewa vizuri mashabiki wa timu hizi mbili kwa uharibifu wao ulikithiri sasa kama hatuutaki huu uwanja basi ngoma hiyo na ipigwe hapo.Sijawahi kuona washabiki wasio wastaaarabu katika medani ya soka kama washabiki wa timu mbili hizi.Hapa ninazungumzuia wale mashabiki wahuni waliokubuhu na wala siyo wote.Hawa mashabiki wao kuingia na chupa za mikoja ni kitu cha kawaida sana kwao,pia uharibifu ni jadi yao mifano ipo kwa pale uwanja wa zamani wa taifa walivyokuwa wakifanya uharibifu pindi timu moja inaposhinda au kushindwa wao ni uharibifu tu.
Ule uwanja ni wa gharama kubwa sana na mashabiki wa simba yanga huwa kwa kweli hawadhibitiki kwa hiyo kama mechi hiyo itapigwa hapo basi juhudi za makusudi zianze sasa jinsi ya kuwadhibiti na pia ufanyike utaratibu kuwa hawa mashabiwasikae pamoja kwa maana kuwa watenganishwe kwani mpaka sasa ule uwanja haujafunguliwa rasmi na haieleweki kuwa mashabiki wa pande zote mbili kuwa pande zao za kukaa ni zipi maana ni tofauti pale tulipokuwa tunashangilia stars wote tulijichanganya na kuwa wa moja sasa je kwa hili serikali na TFF wanafikiria au wanalionaje?
Jitihada za dhati na za makusudi zisipochukuliwa ule uwanja utapata uharibifu mkubwa sana na tutakuja kushangaa kwa jinsi kama hawa mashabiki wasipochukuliwa tahadhari hivi sasa bado mapema.Inawezekana na tujipange sasa kudhibiti mashabiki wahuni wasituharibie uwanja bali timu zao zishindwe zenyewe maana dimba ni kama Emirate mwanawane!

SIMBA NA YANGA SI TIMU KUBWA BALI TIMU KONGWE!

September 29, 2007 by Maka Patrick

Makala ya aliyewahi kuwa kocha wa Simba na Y anga kwa nyakati tofauti Siller Said Mziray leo katika gazeti la Mwanaspoti yamenifurshisha sana, ameandika kuwa timu za Simba na Yanga si timu kubwa katika soka la Bongo bali ni timu kongwe tu nchini ukilinganisha na timu zingine zinazoshiriki ligi ya VodaCom.Kwa kweli ameeleza ukweli mtupu.Ni kama nilivyosema katika makala yangu mojawapo kuwa zile zama za kufikiria kuw Simba na Yanga kuwa wao ndo kila mwaka watakuwa wafalme wa soka katika nchi hii kwa kweli zimepitwa na wakati.Hapa lazima ieleweke kuwa hizi timu hazitofautiani sana kwa kiwango cha soka bali zinazidiana uwezo wa kimaslahi kutokana na kuwa timu hizi ni kongwe na zina wapenzi wengi,wafadhiri wengi na vitu kama hivyo lakini kuhusu soka au kiwango cha kucheza wala havipishani sana na ti.mu zingine zinazoshiriki ligi ya VidaCom.
Hongera Mziray umeongea ukweli mtupu hata kama wadau wengine hawatakubali.Lakini ni sawa kabisa kuwa Simba na Yanga ni wakongwe tu wa soka la Bongo na kamwe wsijindanganye kuwa ni timu kubwa.Timu kubwa hazina wala uwanja wa kufanyia mazoezi achilia mbali mechi,timu kubwa hazina hata utaratibu unaoeleweka kuhusu wachezaji wake na timu kwa ujumla,timu kubwa zinakimbiwa na makocha kila kukicha na mbaya zaidi wanakimbiwa hata na makocha wazalendo je kunani pale Simba na Yanga?Ni ubabaishaji na uswahili mkubwa ndo unatawala pale.Wale wote wanaohusika na majukumu ya timu mbili hizi lazima wasome alama za nyakati na wakubali mabadiliko haraka sana.Simba na Yanga sisi ni wapenzi,wanazi wenu wakubwa kubalini mabadiko hizi ni zama zingine vinginevyo mtakuwa mnarudi nyuma daima badala ya kuenda mbele.Jiulizeni timu kama ElMerreikh miaka michache nyuma ilikuwa timu ya kwaida lakini leo hii angalia jinsi ilivyo angalia jinsi inavyomlipa kocha wake angalia inavyochanja mbuga katika soka la Afrika ina wachezaji wa kulipwa mpaka kutokaBrazil na imepiga hatua sana jamani.SIMBA ,YANGA TUACHE UBABAISHAJI KATIKA SOKA TUKUBALI MABADILIKO ILI HIZI TIMU ZIWE ZENYE KUOGOPEWA NA KUHESHIMIWA HAPA AFRKA HIZI NI TIMU KUBWA JAMANI ACHENI KUZIDHARIRISHA NINYI WADAU NA ACHENI KUWA HAPO KWA MASIRAHI YENU BINAFSI MUWE HAPO KWA FAIDA NA MAENDELEO YA MPIRA WA NCHI HII JAMANI HAKUNA LISILOWEZEKANA KWANI WAO WAWEZE WANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI.WAKATI NI HUU!TWENDE TUJIANDIKISHE SASA!

MASHAMBA YA MIWA YA MTIBWA!

September 29, 2007 by Maka Patrick

Mtibwa Sukari ni eneo linalotoa picha ya kuvutia sana,upande wa mashariki wa eneo hilo limezungukwa na mashamba takribani ekari elfu nne za miwa,kota za wafanyakazi,kiwanda chenyewe cha sukari,miji midogo ya Mabau,Kidudwe,Mji unaokuja kwa kasi wa Madizini,hospitali ya Bwagala,mji wa Turiani mji wa Lusanga pamoja na shule yake maarufu ya sekondari ya Lusanga,chuo cha ualimu Muhonda na maeneo mengine mengi mazuri na ya kupendeza kama Kanga,Dihinda,Kwewmtonga,Mwenvuge,Divumbasa,Mlaguzi Chazi,Kigugu,Mbogo[Mtego wa Simba] Mkindo,Diongoya,Sungaji na maeneo mengi ya kuvutia bial kusahau milima tulivu na inayovutia milima ya Nguu.Kwa kweli maeneo haya yanatoa picha ya kupendeza sana.
Huko kuna timu ya mpira wa miguu ya Mtibwa Sukari ni eneo zuri na tulivu sana lakini kama unafika kwa mara ya kwanzxa unaweza ukataka kurudi leoleo!waja leo warudi leo lakini ukikaa kw siku kadhaa hutatamani kuondoka!Ardhi ina rutuba hali ya hewa nzuri maeneo yanavutia jinsi kulivyo ni kama tukichukua mtaa mmoja wa Dar acha tuseme kama Siza vile ndivyo kunavyofanana mahala pale.Nimewahi kuishi kule hususan maeneo ya Chazi Hospitali na nimekuwa na ndoto ya kuishi maeneo yale kwa maana yananivutia sana.Hata Salome Ihembe a.ka. Salome Leng’alwa analitambua hilo.Tukijaaliwa katika siku za usoni ninapenda sana kuhamishia makazi yangu huko,Turiani,Chazi,Mtibwa na maeneo ya jirani kwa kweli kwangu mimi yanatoa picha ya kupendeza sana.Salome upo!Mtibwa Sukari na hatima ya soka la Tanzania!Wasalimie Manungu!

MSAFIRI KAFIRI!

September 29, 2007 by Maka Patrick

Jumamosi leo wiki endi mapumziko kwa wengi wetu baada ya wiki nzima ya kuchakarika na kazi zinazotuhusu,watu ni wengi Kariakoo,Posta,mitaa ya Kisutu na kila kona ya jiji.Kila mtu anajaribu kupata kile kilichomtoa nyumbani mchana huu.Madukani ni mshikemshike sokoni Kariakoo ndo usiseme,mtaa wa Msimbazi ni balaa tupu kuna mabasi mawili yamekodishwa na wapenzi wa Simba wanaojiita matawi ya mpira pesa wanajinadi kuwaeleza abiria kuwa usafiri upo wa kwenda Mji kasoro bahari kushuhudia pambano la mpira kati ya Simba na timu ya Pan Afrian[Twiga] ya Kinondoni.
Napita katika maduka ya TV nataka kununua TV maana ligi ya Uingereza siku hizi tunaifaidi kupitia TV ya Taifa shukurani kwa Tido Mhando kuwezesha sisi walala hoi kuona mpira wa kweli.Wauzaji wote hakuna anayesema ukweli kila mtu anavutia kwake unajua kilichotokea nimeamua kuachana na manunuzi ya TV nitanunua ya mtumba lakini sizipendi kwa kuwa zinachangia kuchafua mazingira ya hapa Bongo maana kwa nini zije huku wakati huko kwao zimeishatumika kwa nini watuletee siosi?Basi sitanunua kabisa!Ukipita madukani wote wanauza wanatumia lugha nzuri sdana na wana nidhasmu ya hali ya juu huwezi amini.Kweli sasa hivi Bongo biashara ni biashara huria!
Nimechoka kuzunguka madukani nipo Rik Pub nyuma ya jengo la Washirika nimeagiza msosi unapigwa wiombo wa Msafiri Kafiri navutiwa nao maana mimi ni penzi wa Msondo si unakumbuka jana nimeelezea kuhusu wimbo wa Msondo wa Nidhamu ya Kazi?
Hapa unapigwa Msafiri Kafiri kwa kweli nimechanganyikiwa mimi ni Mnazi mkubwa sana wa Msondo:
Msafiri kafiri mwenda pole hajikwai akijikwaa haumii kuumia kwake kidogo tuu
Mimi msafiri kafiri nakuja nawapisha wale waendao na warudio kwa haraka mimi naja taratibu!Msondo NGOMA YA wATANZANIA!WANACHEZEA UMEME HAO WATANASA SASA HIVI!

NIDHAMU YA KAZI.

September 28, 2007 by Maka Patrick

Msondo ngoma baba ya muziki wana magoma kitakita wale jamaa kiboko kwa tunzi zao mbalimbali.Nyimbo kama “NIDHAMU YA KAZI” kwa kweli ni moja ya nyimbo zenye ujumbe mzuri sana kwa jamii.Maana kazi ndiyo msingi wa maendeleo,kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa “Kazi ndiyo msingi wa maendeleo,nchi masikini haiwezi kuendelea kama inategemea fedha kuwa ndiyo msingi wa maendeleo,nchi masikini haiwezi kuendelea kama inategemea misaada kutoka nchi za nje”Maneno haya aliyasema wakati anafungua uwanja wa Mapinduzi[uwanja wa Sokoine]Mbeya.
Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio mema kazini
Viongozi na wafanyakazi lazima sote tuwe na nidhamu
Migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu
Viongozi pia wajibu wenu mkubwa ni kulinda heshima
N kudumisha nidhamu ya kazi
Haya yote ni rahisi kuapatikana iwapo tutatia maanani suala la nidhamu!

SHULE YA MSINGI KIGUGU-2

September 27, 2007 by Maka Patrick

Habari hii nimeitoa kwa ufupi lakini bado ninaitafutia muda ili niiandike kwa kirefu kwani ni habari ndefu kidogo ambayo ina mambo mengi sana yaliyotukia enzi hizo tukiwa shule ya msingi Kigugu kule Chazi Turiani Morogoro Vijijini enzi hizo siku hizi ni wilaya ya Mvomero.
Nitakuja na majina ya ajabu ya wanafunzi tuliosoma nao kama Veronika Mezanyoka,Augustino Mkeka,Rose Mdudu Chanzala ThomasSamboa Akisa,na jamaa aliyeibia wakati wa mtihani akaandika mpaka jina la yule aliyekuwa akiibia mtihani wake!

MADEREVA,MAKONDA VS WANAFUNZI!

September 27, 2007 by Maka Patrick

KITUO CHA KARUME:
DALADALA:TABATA-SEGEREA:
MUDA:JIONI:
Wakazi wa Segerea wengi wetu lazima tupandie hapo Karume tukageuze na basi mpaka mnazi Mmoja mana usafiri wa Segerea ni taabu kwelikweli.Konda kasimama mlangoni tunaingia bila wasiwasi maana si twaenda kugeuza nalo,tunalipa mara mbili “Kongo Mnazi ikirudi Segerea!”Konda kamuona mwanafunzi hana makuu mwanafunzi yule mpole konda anamzuia mlangoni dogo anafanikiwa kuingia anakaambele kwa dereva mahala pasipo na kiti,nmi nipo mbele dereva “Mangi” anaanza kumfokea kwa nini unafanya vurugu mlangoni ukiumia nani atakulipa?Anamtukana dogo kakaa kimya tu kachoka na anaonyesha woga.Naingilia kwani kafanyaje?Anajibu hujamuona kafanya vurugu mlangoni namuuliza vurugu gani maana konda kamzuia sasa angeingiaje?Anajibu wewe unatetea ujinga wewe mpumbavu namjibu wewe ndo mpumbavu maana mtoto hajafanya vurugu unasema kafanya vurugu.Tunajibizana mpaka mnazi.Pale watu kibao sasa ndo wanafanya vurugu za kweli na wanaweza kuumia kwa kugombania basi namtazama dereva kwa chati halafu nacheka sana sana mpaka watu wananishangaa nafikiri jibu amelipata kwa nini ninacheka ni kuwa je wale watu wote wakiumia kwa kugombania basi atawalipa?Maana wamefanya vurugu n yule dogo pale Karume hakufanya vurugu kaambiwa kuwa anafanya vurugu akiumia nani atamlipa?
Wanafunzi wanapata taabu sana katika jiji hili hasa nyakati zza asubuhi na jioni,wanakatazwa hata kukaa hata kama basi halijajaa.Ugomvi wa kijana yule na koda na dereva kisa ni 50/= anayolipa ndiyo inamfanya asithaminiwe utu wake.Lakini si yeye anayepanga bei hiyo yeye anaathiriwa na mfumo tu jamani.
Na nimechunguza sana madereva na makonda vijana ndiyo wanawanyanyasa vijana wenzao wadogo zao.Lakini fanya utafiti utagundua kuwa makonda na madereva watu wazima wenye familia kamwe hawawanyanyasi wanafunzi na iwapo imeshindikana kuwachukua watawaeleza kistaarabu,binafsi nimewahi kumshuhudia konda wa makamo akiwakataa watu wazima na kuwachukua wanafunzi watoto wadogo nyakati za jioni ili wawahi nyumbani!Iinapaswa wengine waige mfano huo japo kwa kutoa lugha ya kistaarabu jamani.